Mwanaume mwenye mke na watoto wawili amekamatwa Wilayani Burera kwa tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 15 juma pili.
Mashahidi wamesema alimbaka mtoto huyo baada ya kuahidi atampa nyasi za mifugo.
"Alimkuta alipokuwa akitafuta nyasi za mifugo na kumuahidi akuje atampa nyingine zaidi. Alimbaka walipofika kichakani na kumbabaisha kuwa akipiga mayowe atamkata kwa mpanga." mkazi ameambia Umuseke
Msemaji wa Ofisi ya Uendeshamashtaka nchini Rwanda (RIB), Umuhoza Marie Michelle amethibitisha taarifa hizo na kutangaza kuwa upelelezi kuhusu kesi hii umeanzishwa.
Akionekana kuwa na hatia, mtuhumiwa atafungwa miaka jela kati ya miaka 20-25.
Isangize abandi
Tanga igitekerezo