Mkazi Wilayani Gisagara, Tarafa ya Save Kijijini Syanda, Clementine Mukeshimana ameonekana mbele ya Gavana wa Mkoa wa Kusini, Emmanuel Gasana akiwa na malalamiko ya kunyanganywa ng’ombe aliyepatiwa na serikali kwa mradi wa ’ Gira Inka’ kumaanisha " Miliki ng’ombe’
Mkuu wa Kijiji, alimuambia Gavana tarehe 5 Novemba kwamba Mukeshimana alinyimwa ng’ombe wake kwani hakuwa na zizi.
Hata hivyo, majirani walisema huo ni ungo mtupu. Wameambia Ukwezi.com kuwa alipokutana na gavana Gasana, Mukeshimana alikuwa ametimiza wiki tatu akiwa na zizi.
Majirani wamesema zizi lake Mukeshimana halina paa na ndio maana hajapatiwa ng’ombe kinyume na alichoagiza Gavana Gasana.
Isangize abandi
Tanga igitekerezo