Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC), Bw John Bosco Kalisa, amewataka wajasiriamali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo), kujiunga na baraza hilo ili kupata faida nyingi zinazotolewa kwa washiriki.
Bw Kalisa alisema hayo jana tarejhe 9 Mai wakati wa kufungua rasmi mkutano kati ya EABC na Shilikisho la wajasiriamali nchini Jamhuri ya Kidemukrasia ya Congo, hotelini Linda, mjini Goma.
Kiongozi huyo amesema huu ni wakati wa FEC kujiunga na EABC baada ya Jamhuri ya Kidemukrasia ya Congo kuwa mmoja mwa washiriki wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
" Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni mshiriki wa EAC. Tunawataka watu wa sekta binafsi, wajasiriamali kujiunga na EABC ili kupata faida wanazopata washiriki wengine. Hili litasaidia tena kupata fursa biashara na uwekezaji kati nchini nyingine sita." Kalisa amesema
Amewaambia pia waliohudhuria huo mkutano kuwa ufanyabiashara kati ya nchi za EAC na DR Congo uko kwa kiwango kidogo sana, ukilinganisha kama vile nchi hio inafanya na Afrika Kusini.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo mara nyingi inajulikana kama jitu kubwa la Afrika, inatoa fursa kubwa ya kibiashara. Ina takriban watu milioni 81, inashikilia karibu nusu ya nchi wanachama wa EAC, na hivyo kuwa na soko kubwa. Hadi sasa, karibu nusu ya biashara kati ya DRC na EAC si rasmi, ikimaanisha kuwa uwezekano wa biashara haujaimarishwa. Licha ya ukaribu wake wa kijiografia, biashara ya DRC na EAC ni ya kushangaza sana."
La kushangaza lakini, kiwango cha biashara kati ya nchi za EAC na DRC ni 13.5%, jambo ambalo amesema linastahili kujadiliwa vilivyo kwa kupunguza hio pengo.
Hata hivyo, manamo mwaka 2018, Rwanda iliongoza nchi za EAC kufanya biashara zaidi na EAC. Kwa hili, inafuata Uganda, Tanzania, Kenya na Burundi.
CEO wa EABC John Bosco Kalisa
John Bosco Kalisa amesisitiza kwamba EABC inajitolea kuwezesha uwezekanaji wa kufanya biashara katika jumuiya na itafanya lolote kuzitatua changamoto inazowakabili washirika wake.
Emmanuel Nkusi, Mjumbe wa Bodi ya EABC amesema kuwa mkutano huo " Muhimu kufahamisha mageuzi ya sera yanayohitajika ili kurahisisha biashara ya mipakani."
Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) ni chombo kikuu cha vyama vya Sekta ya Kibinafsi na Mashirika kutoka Nchi sita za Afrika Mashariki.
Ilianzishwa mwaka 1997 ili kukuza maslahi ya Sekta Binafsi katika mchakato wa mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ikijumuisha wanachama kutoka Kenya, Tanzania na Uganda, uanachama wake ulipanuliwa baada ya 2007 na kujumuisha Sekta Binafsi kutoka Burundi, Rwanda na Sudan Kusini mnamo 2016.
Kuna matatizo yanayowakabili wafanyabiashara katika EAC. Baadhi wanakashifu changamoto katika kuvuka mipaka, harakati za wafanyakazi, ushuru na kadhalika.
Tanga igitekerezo