Mtoto wa miaka 10 amemwambia mfanyakazi wa kituo cha kulelea watoto kuwa anataka kuwa mfanyabiashara ya madawa kulevya.
Mtoto huyo aliripotiwa kuwa na uelewa mkubwa wa aina za madawa ya kulevya, katika uwasilishaji wa ripoti mfanyakazi wa kituo hiko alieza tabia za mtoto huyo.
Mkuu wa kituo hiko aliezea kuwa kunahitajika mikakati ya mara moja kupambana na tatizo kama hilo.
Polisi inasema kuwa vijana wengi wanaona kuwa kazi ya madawa ya kulevya kuwa ni jambo la usasa.
’’Tuna vijana wengi ambao wamekua wakitaka kufanya kazi za dawa za kulevya ’’ anasema Leona Dinsdale msemaji wa polisi YMCA.
’’Tulikua na kijana mmoja ambaye anataka kufanya kazi hii, familia yake ilikua inahusika na biashara haramu na kumsababisha aone ni jiambo la kawaida, ana miaka kumi tuu na anaweza kueleza aina zote za dawa za kulevya, mfano cocaine na heroin zote anazijua’’ anaongeza Dinsdale
anasema kuwa alipitia programu ya wiki nane na baadae taratibu akaanza kuelewa umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii.
Chama kimoja cha kujitolea kinasema kuwa lengo kwasasa ni kuhakikisha wanapambana na tabia za kihalifu hasa kwa watoto.
Suala hili mara nyingi linahusishwa na nchi ambapo wahalifu huweza kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu na huwalenga sana makundi yenye kuweza kushawishiwa haraka ikiwemo watoto, na pia huongeza mtandao wao kutoka mjini kwenda vijijini.
Alisa Newman kutoka kituo cha polisi cha Yorkshire anasema kuwa vijana wengi wanapenda kazi kama hizo , na hajui kukataa wala kusema hapana kwa nafasi kama hizo pale wanaposhawishiwa.
Chanzo: BBC
Tanga igitekerezo