Wanaumwe Wilayani Nyamasheke, magharibi kusini mwa Rwanda wameweka wazi kuwa wananyanyaswa na wanawake wao wanaowazidi mali.
" Kuna wakati ambapo mwanaume hana cha kusema nyumbani. Mwanamke amekwenda kazini kisha akaenda baani bila kukumbuka amemuacha nyumbani mumewe akiela watoto. Nadhani kuwa huyo mwanaume ananyanyaswa." Ameambia Igihe mmoja mwa wanawake, Mukakageruka Séraphine
" Mwanamke akiwa na fedha hawezi kukbali wewe useme lolote. Kuwa na kazi kwake siyo vibaya lakini kuna wakati ambapo anakwenda na anarudi saa tanu usiku, na wewe kama mwanaume huwezi kusema chochote." Amesema mwanaume, Ntamarerero Félicien.
Mukamana Claudette, Afisa kwa wajibu wa Mambo ya Kijamii Wilyani Nyamasheke amesema kunyanyaswa kwa wanaume kunatokana na kutosema hadharani matatizo yanayowakabili.
Kiongozi Mukamana amewataka wanaumwe wasikae kimya kuhusu unyanyasaji wanaofanyiwa.
Tanga igitekerezo