Kigali: Wanaosubiri msaada wa serikali wapia mayowe
Wakazi Tarafa la Bumboko kijijini Ngara wametangaza kukumbwa na njaa baada ya kusubiri msaada wa serikali wakaukosa wakati wa kutotoka nyumbani kwa ajili ya Virus vya Corona.
Baadhi yao wameambi Bwiza.com kuwa waliandikwa na viongozi wao wiki iliyipita ila bado hawajapokea kitu.
" Waliandika majina yetu wiki iliyopita, wengine wamepata chakula lakini sisi hatujapokea." Mmoja wao aliyeomba kutojuliakana amesema
" Kuna taarifa kuna chakula kwenye tarafa lakini hatujapata, kwa nini" mwingine ameongeza
Kwa ujumla, wakazi hawa wanadai kuna wasiwasi kubwa kutokana na kuwa siku za kubaki nyumbani zimeongeza hadi tarehe 19 Aprili mwaka huu.
Katibu Mtendaji wa Tarafa ya Bumbogo, Deo Rurangirwa amekubali madai ya wakazi.
" Kuna wale ambao hawajapata. Tulianzia kwa wale ambao walikuwa wanahitaji msaada kuliko wengine." amesema
Hata hivyo, amepiga maruku kuwa kuna chakula kilichohifadhiwa na viongozi kwenye tarafa kama wanavyosema wakazi.
Kiongozi huyo amewataka wakazi kusubiri na kuwahamasisha wale wenye uwezo kuwasaidia wenzao.
Leave a Comment