Zaidi ya 40 wameuawa katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao mashariki mwa DR Congo


Swahili

Wanamgambo wa kundi linalojulikana kwa jina la Codeco (Cooperative for Development of the Congo) leo wamelaumiwa kwa shambulio kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kusababisha zaidi ya watu 40 kuuawa.

Maafisa wa eneo hilo walisema kundi hilo lilivamia kambi ya Lala mapema Jumatatu; waliwafyatulia risasi wakazi kabla ya kuchoma moto vibanda.

Baadhi ya waliokuwa ndani walichomwa moto hadi kufa.

Ni shambulio la hivi punde zaidi la kundi hilo, ambalo linadai kutetea maslahi ya wakulima wa Lendu.

Makumi ya maelfu ya watu wamekimbia vijiji vya pembezoni katika wiki za hivi karibuni kutafuta hifadhi katika mji wa Bule, ambako kuna walinda amani wa Umoja wa Mataifa.



Habari...

Leave a Comment

Who are you?
Your post
  • This form accepts SPIP shortcuts [->url] {{bold}} {italic} <quote> <code> and the HTML code <q> <del> <ins>. To create paragraphs, simply leave blank lines.

Kibarua cha habari