trump10

Trump Aahidi Kutwaa Gaza na Kuwahamisha Wapalestina Kwingineko.

Sangiza iyi nkuru

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kwamba Amerika “itaitwaa” na “kuiweka chini ya umiliki wake” Gaza baada ya kuwahamisha Wapalestina sehemu nyingine, katika mpango wa kipekee alioueleza kuwa unaweza kuibadilisha eneo hilo kuwa “Riviera ya Mashariki ya Kati.”

Rais Trump alitangaza mikakati hii mipya ya nchi yake kwa Mashariki ya Kati bila kutoa maelezo zaidi, wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Kabla ya kutangaza hatua hizi, Trump aliwashangaza wengi alipodokeza kwamba Wapalestina wa Gaza wanapaswa kuhamishwa kwa kudumu kwenda nchi jirani.

Rais Trump alieleza kwamba Amerika itachukua Gaza na kuanzisha miradi ya maendeleo huko.

Mbele ya waandishi wa habari alisema: “Tutaifanya iwe yetu, na tutafanya kila kitu kinachohitajika ili kuharibu na kulipua mabomu yaliyopandikizwa na silaha zingine.”

Netanyahu, aliyemsifu Trump kama “rafiki mkubwa zaidi” ambaye Israel imewahi kuwa naye, alisema kuwa mpango wa Rais wa Marekani unastahili “kufikiriwa” na unaweza “kubadilisha historia.”

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *