GridArt_20250523_74154312_copy_1000x666

Jenerali wa Karibu na Kabila Akamatwa Wakati Serikali Yazidi Kumwandama

Sangiza iyi nkuru

Brigedia Jenerali Pierre Banywesize, mshirika wa karibu wa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila Kabange, amekamatwa.

Banywesize alikuwa mlinzi wa karibu wa Joseph Kabila.

Ripoti zinaeleza kuwa alikamatwa Alhamisi, Mei 22, na idara ya ujasusi ya DRC, muda mfupi baada ya kuhojiwa.

Jenerali huyu, ambaye alikuwa akihudumu kwa muda mrefu huko Dungu, jimboni Haut-Uele, anaripotiwa kukamatwa akiwa Kinshasa, alipokuwa akisubiri kusafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Hadi sasa, haijajulikana ni makosa gani anashitakiwa nayo.

Hata hivyo, kukamatwa kwake kunakuja wakati serikali ya Kinshasa inaendelea kuwasaka waliokuwa wandani wa Kabila.

Alhamisi, Seneti ya DRC ilimvua Kabila kinga ya kisheria, na kuruhusu Mahakama Kuu ya Kijeshi kumfungulia mashtaka ya kushiriki katika kundi lililokuwa linapanga kupindua serikali ya Rais Tshisekedi, uhaini, pamoja na kushiriki katika makundi yanayofanya uhalifu wa kivita na dhidi ya binadamu.

Serikali ya Kinshasa imekuwa ikimtuhumu Kabila kwa muda mrefu kuwa anashirikiana na kusaidia waasi wa M23 ambao wanaendelea kupigana na serikali.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *