Katika jiji la Harare, nchini Zimbabwe, wanawake watatu wanaodaiwa kuwa makahaba pamoja na mwanaume mwenye mke mjamzito, walikamatwa wakifanya mapenzi hadharani usiku katika eneo la Southlea Park.
Kwa mujibu wa gazeti la H-Metro, tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 9 Juni 2025, majira ya saa tatu usiku, baada ya polisi kupokea taarifa.
Polisi walifika eneo hilo wakiongozwa na Konstebo Precious Manyimbiri, wakishirikiana na Sajenti Dohwe na maafisa wengine wawili, na kuwakuta wakiwa katika tendo la ngono.
Waliohusika ni Mellisa Mapanga (miaka 23), Rutendo Joseph (miaka 27), Elsie Mupesa (miaka 22), na Takura Pedzisai (miaka 35). Wanawake hao walikiri kuwa wanafanya ukahaba kama njia ya kujipatia riziki.
Walipofikishwa mbele ya mahakama ya Mbare, wote walikubali kosa la utovu wa nidhamu hadharani. Jaji Tatenda Mukurunga aliwaamuru kila mwanamke kulipa faini ya $50 au kufungwa kwa siku 45 iwapo hawatalipa. Pedzisai alitozwa faini ya $100 kutokana na uzito wa kosa hilo kwa kuwa mke wake ni mjamzito.
Jaji aliwakumbusha wananchi kwamba tabia chafu hadharani haitavumiliwa, akihimiza watu kudumisha maadili ya kitamaduni na kuilinda heshima ya maeneo ya umma.


