241218-img-nicolas-sarkozy-legion-d-honneur-1

Sarkozy Aondolewa Tuzo ya Heshima ya Taifa la Ufaransa Baada ya Kupatikana na Hatia

Sangiza iyi nkuru

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, aliyelitawala taifa hilo kati ya 2007 na 2012, amevuliwa tuzo yake ya heshima ya “Légion d’honneur” baada ya kupatikana na hatia, kwa mujibu wa amri iliyotangazwa Jumapili.

Sarkozy anakuwa kiongozi wa pili wa taifa la Ufaransa kupokonywa tuzo hiyo ya juu kabisa baada ya Philippe Pétain, aliyekuwa kiongozi wa serikali ya Vichy wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, ambaye alihukumiwa kwa usaliti na kushirikiana na Wanazi mnamo Agosti 1945.

Uamuzi huu uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu umetolewa licha ya Rais wa sasa Emmanuel Macron kusema mwezi Aprili kwamba anaamini ni muhimu “kuwaheshimu marais wa zamani.”


Kwa nini Sarkozy amepokonywa tuzo hiyo?

Tuzo ya “Légion d’honneur”, ni heshima ya juu kabisa nchini Ufaransa inayotolewa kwa raia wa kawaida na wanajeshi, na ilianzishwa mwaka 1802 na Napoleon Bonaparte.

Kwa mujibu wa sheria zake, mtu yeyote anayepatikana na hatia au kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja au zaidi hupoteza tuzo hiyo moja kwa moja.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *