Ali_Shadmani_iran_1750146291848_1750146292005 (1)

Israeli Yamuua Jenerali Mkuu wa Iran Katika Shambulio la Angani

Sangiza iyi nkuru

Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) limetangaza siku ya Jumanne kwamba limemuua Ali Shadmani, jenerali mkuu zaidi wa Iran wakati wa vita.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa X (zamani Twitter), IDF ilimwelezea Ali Shadmani kuwa “jenerali wa ngazi ya juu kabisa nchini Iran na mshauri wa karibu wa Kiongozi Mkuu Ali Khamenei.”

IDF iliongeza kuwa Shadmani aliuawa katika shambulio la angani lililofanywa katikati ya jiji la Tehran, baada ya kupata “taarifa za kiintelijensia zisizotia shaka.”

Ali Shadmani alikuwa amepewa wadhifa huo hivi karibuni, akichukua nafasi ya Alam Ali Rashid, aliyeuawa mapema mwezi huu.

Kifo chake kinaongeza idadi ya maafisa wa jeshi la Iran waliouawa na Israel katika kipindi cha siku tano zilizopita, akiwemo Kamanda wa Vikosi vya Ardhi, Mkuu wa Majeshi, Kamanda wa Jeshi la Anga, Mkuu wa Ujasusi, na wengine wengi.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *