Katika kesi ya Sean ‘Diddy’ Combs, rapa maarufu duniani, majaji walipewa video yenye jina “Freak Offs” inayodaiwa kuonyesha biashara ya wanawake na tendo la ngono la waziwazi.
Kulingana na Mail Online, video hiyo inaonyesha Diddy akiwa na watu wengine, wakiwemo mpenzi wake wa zamani Cassie Ventura. Video hiyo ilipigwa Oktoba 2012 katika chumba cha Trump International Hotel, New York, ikimuonyesha Ventura akiwa na wanaume wawili wanaojulikana kama ‘The Punisher’ na Dave.
Video hiyo ilionyeshwa kwa majaji pekee, waliotumia headphones kusikiliza muziki na mlio wa wanawake.
Kutokana na maudhui ya kutisha, baadhi ya majaji walionyesha ugumu wa kuvumilia yaliyokuwa yanaonyeshwa, baadhi wakajifunika uso.
Jaji Arun Subramanian aliamuru video hiyo ibaki kuwa siri baada ya pande zote mbili – utetezi wa Diddy na upande wa Cassie – kuomba isitumike hadharani.
Kesi hiyo inaendelea kuvutia watu wengi duniani kutokana na mashtaka makubwa ya biashara ya watu, ukatili wa kijinsia na mateso yanayohusishwa na Diddy.


