Marekani inapanga kuongeza nchi 25 kutoka Afrika kwenye orodha ya zile ambazo raia wake wamezuiwa kabisa kuingia kwenye ardhi ya Marekani.
Nchi hizi za Afrika ni sehemu ya mataifa 36 ambayo Washington inakusudia kuweka kwenye orodha mpya, kwa mujibu wa nyaraka ya ndani ya serikali ya Marekani iliyopatikana na vyombo vya habari vya Washington Post na Reuters.
Nyaraka hiyo ilisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, mnamo Juni 14 na kutumwa kwa mabalozi wa nchi husika ili kuwafahamisha uamuzi huo mpya.
Hata hivyo, mataifa hayo yamepewa muda wa siku 60 kutimiza masharti ya Marekani ili kuepuka kuingia kwenye orodha nyeusi.
Washington imesema hatua hii inalenga hasa nchi ambazo haziwezi kutoa “vitambulisho vya kuaminika,” au zile zilizo na “rushwa kali ya utawala.”
Pia inahusu mataifa yenye idadi kubwa ya raia waliopo Marekani kinyume cha sheria kuliko idadi ya viza zilizotolewa rasmi.
Nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ziko hatarini, isipokuwa Rwanda na Kenya.
Kwa ujumla, nchi za Afrika zilizoorodheshwa ni Angola, Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Cameroon, CĂ´te d’Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Djibouti, Ethiopia, Misri na Gabon.
Pia zimo Gambia, Ghana, Liberia, Malawi, Mauritania, Niger, Nigeria, SĂŁo TomĂ© na PrĂncipe, Senegal, Sudan Kusini, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.
Mwanzoni mwa mwezi huu, Marekani ilikuwa imeshatoa orodha ya nchi 12 ambazo raia wake wamepigwa marufuku kabisa kuingia nchini humo, ikisema inalenga “magaidi wa kigeni.”
Nchi hizo ni Afghanistan, Myanmar, Chad, Congo-Brazzaville, Guinea ya Ikweta, Eritrea, Haiti, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen.
Wakati huo huo, Washington ilieleza kuwa kuna nchi saba ambazo raia wake walizuiwa kwa kiasi na Rais Donald Trump kwa sababu walichukuliwa kuwa “hatari kubwa” kwa Marekani.
Nchi hizo ni Burundi, Cuba, Laos, Sierra Leone, Togo, Turkmenistan na Venezuela.


