_132928382_gettyimages-2071909768-removebg-preview

Putin: Iran Ilikataa Ushirikiano wa Ulinzi wa Anga Tuliowapa

Sangiza iyi nkuru

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, katika mkutano na viongozi wa mashirika makubwa ya habari duniani ulioandaliwa na Shirika la Habari la Urusi, TASS, alisema kwamba Urusi iliipatia Iran fursa ya kushirikiana kwenye miradi ya ulinzi wa anga, lakini Tehran haikuonesha ari kubwa.

Putin alisema:

“Kama mnavyojua, tuliwahi kuwapatia marafiki wetu wa Iran nafasi ya kushirikiana katika mpango wa ulinzi wa anga. Wakati huo, washirika wetu hawakuonesha kuwa na hamasa. Kuhusu makubaliano ya ushirikiano mliyoyataja, hayana vipengele vya kijeshi. Hilo ni jambo la pili. La tatu, marafiki wetu wa Iran hawajayataka. Kwa kifupi, hakuna jambo la kujadili.”

Usiku wa Juni 13, Israel ilianzisha Operesheni Rising Lion, iliyolenga kuvuruga mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia wa Iran. Ndani ya masaa 24, Iran ilijibu kwa mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Katika siku zilizofuata, Tel Aviv na Tehran waliendelea kurushiana makombora na ndege zisizo na rubani (drones). Pande zote mbili zilithibitisha kuwepo kwa vifo, na kila upande uliahidi kushambulia zaidi, ingawa hazikutangaza uharibifu halisi uliotokea.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *