Serikali ya Rwanda imetoa likizo ya siku sita kwa watumishi wote wa umma, ikijumuisha siku mbili za wikendi, kwa heshima ya Siku ya Uhuru na Siku ya Ukombozi.
Jumanne, Julai 1 itakuwa ni Siku ya Uhuru, na Ijumaa, Julai 4 itakuwa ni Siku ya Ukombozi.
Mbali na hizi sikukuu mbili rasmi, Wizara ya Utumishi wa Umma na Kazi imetangaza kuwa Jumatano, Julai 2 na Alhamisi, Julai 3 pia zitakuwa siku za mapumziko.
Hii ina maana kwamba katika wiki inayoanza Juni 29, watumishi wa umma watafanya kazi siku moja tu ambayo ni Jumatatu, Juni 30.
Taarifa ya Wizara pia imesema kuwa kazi zitaanza tena rasmi Jumatatu, Julai 7.
Hata hivyo, wizara imesisitiza kuwa huduma muhimu zitaendelea kutolewa ili kuhakikisha kuwa shughuli za msingi hazisimami.

Siku ya Ukombozi ni moja ya sababu kuu zilizofanya serikali kutoa likizo ya wiki nzima.


