histo

Twirwaneho Yatoa Onyo Kuhusu Mashambulizi Yanayolengwa Kwa Wabanyamulenge Minembwe

Sangiza iyi nkuru

Kikundi cha waasi cha Twirwaneho, kinachodai kulinda raia wa Congo wenye asili ya Kinyamulenge, kimetoa tahadhari kuhusu mashambulizi makubwa yanayodaiwa kuandaliwa na muungano wa jeshi la FARDC, waasi wa FDLR, wanamgambo wa Wazalendo, na wanajeshi wa Burundi.

Katika taarifa yao, kikundi hicho kinasema kwamba muungano huo umezingira maeneo ya Minembwe, ukianzisha kambi za kijeshi na kujiandaa kufanya mashambulizi ya ardhini na ya anga.

Twirwaneho kinadai kuwa jeshi la serikali linatesa na kufukuza jamii za Banyamulenge kutoka maeneo yao ya asili.

Pia wanasema kuwa ndege za kivita aina ya Sukhoi na drones zinajiandaa katika Kisangani na Bujumbura kwa lengo la kulenga kambi zao na vijiji vya raia, kwa madai ya kupambana na “makundi yenye silaha”.

Lt. Jenerali Pacifique Masunzu anatajwa kuwa mratibu mkuu wa operesheni hiyo, kwa kushirikiana na maafisa wakuu wa jeshi la Burundi, na Minembwe ikitajwa kuwa kituo kikuu cha mashambulizi.

Twirwaneho wanadai kuwa mashambulizi haya ni zaidi ya harakati za kijeshi; ni mpango wa mauaji ya kikabila, na kuna hatari ya mauaji ya halaiki.

Wanasema hawatakaa kimya wakitazama jamii ya Banyamulenge ikiteketezwa, bali watachukua hatua za kujilinda.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *