Tarehe 13 Juni 2025, Israel ilianzisha Operesheni kubwa iliyopewa jina la Rising Lion, ikishambulia viwanda vya kemikali na vituo vya kijeshi vya Iran—ikiwemo Natanz, eneo muhimu ambapo Iran hufanya utafiti wa urani kwa ajili ya kutengeneza silaha za nyuklia. Wachambuzi wanasema Israel inalenga kuzuia mipango ya Iran kutengeneza silaha za maangamizi.
Iran haikukaa kimya. Ilijibu kwa kutuma droni zaidi ya 100 kushambulia ardhi ya Israel. Hii inatokea baada ya mashambulizi makubwa mnamo 2024, ambapo Iran ilirusha makombora na ndege za kivita zaidi ya 300, nyingi zikiwa zilikamatwa angani.
Wataalamu wa unabii wa Biblia kama Greg Laurie wanasema matukio haya yanafanana na yale yaliyotabiriwa kwenye Ezekieli 38–39, ambapo Uajemi (Iran ya leo) itashirikiana na mataifa yenye nguvu kutoka kaskazini kumpinga Israeli.
Laurie anasema ingawa haya siyo utimizo kamili wa unabii huo, yanaweza kuwa mwanzo wa mfululizo wa matukio yajayo. Biblia pia ilitabiri kwamba Israeli itarudi kwenye ardhi yake (ilivyotokea mwaka 1948), itakuwa na maadui wengi, na itaishi katika hali ya mateso—ambayo sasa ni hali halisi.
Waumini wa Biblia wanahimizwa wasikate tamaa, bali wawe tayari kiroho. Laurie anasisitiza maneno ya Yesu:
“Mkiyaona haya yakitokea, inueni vichwa vyenu juu, kwa maana ukombozi wenu umekaribia.” (Luka 21:28)
Haya yanajiri wakati unabii wa Biblia unatoa onyo kwamba Uajemi (Iran) itakuwa miongoni mwa mataifa yatakayompinga Israeli katika siku za mwisho. Je, haya ni dalili kuwa tupo karibu na hayo maandiko kutimia? Wengi bado wanasubiri, lakini jibu la kweli limo mikononi mwa Mungu.


