kanyuka_lw-3b911

AFC/M23 Yaituhumu Serikali ya DRC kwa Kuua Wanachama Wanne Wakati wa Mazungumzo ya Amani

Sangiza iyi nkuru

Kikundi cha waasi cha AFC/M23 kimelishutumu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa kuwaua wanachama wake wanne, kikieleza kuwa kitendo hicho ni ishara ya uchokozi wa vita, licha ya mazungumzo ya amani yanayoendelea kati ya pande hizo mbili.

Msemaji wa AFC/M23, Lawrence Kanyuka, alisema wanajeshi wa serikali waliwaua watu hao katika Jimbo la Kivu Kusini.

“Tarehe 12 Julai 2025, wanajeshi wa taifa waliwaua ndugu zetu wanne katika eneo la Cirunga groupement. Hii inaonyesha wazi kuwa serikali haitilii maanani mazungumzo ya amani na ina nia mbaya,” alisema Kanyuka.

Kwa mujibu wa jamii ya kiraia ya eneo la Kabare, kati ya waliouawa walikuwemo walimu wawili wa shule ya msingi ya Kabare 1, waliokuwa wametoka kwenye kituo cha ukusanyaji wa mitihani cha kitaifa kilichoko Canya.

Kanyuka pia alionya watu wa Kongo na jumuiya ya kimataifa kwamba serikali ya DRC inaendelea kupeleka wanajeshi na silaha nzito karibu na ngome za AFC/M23, jambo linaloashiria maandalizi ya vita.

AFC/M23 imeonya kwamba vita vinaweza kuzuka ikiwa DRC itaendelea na maandalizi ya kijeshi huku mazungumzo yakiendelea huko Qatar.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *