Waziri wa Ujasusi wa Iran, Esmail Khatib, ametangaza kwamba Tehran iko tayari kufichua hivi karibuni nyaraka nyeti zilizodaiwa kuibwa kutoka Israel, zinazoonyesha silaha zake za nyuklia, uhusiano wake na Marekani, Ulaya na mataifa mengine, pamoja na uwezo wake wa kujilinda.
Khatib aliyasema hayo Jumapili kupitia Televisheni ya Taifa, akieleza kuwa nyaraka hizo ni “hazina” inayoweza kuimarisha nafasi ya Iran kimataifa, japo hakutoa ushahidi wowote.
Serikali ya Israel — ambayo inadaiwa kuwa nchi pekee Mashariki ya Kati yenye silaha za nyuklia — haijatoa tamko lolote kuhusu madai ya kuibwa kwa nyaraka hizo, kwa mujibu wa Al Jazeera.
Hata hivyo, baadhi ya raia wa Israel wanaodaiwa kuwa wapelelezi wa Tehran wakati wa vita vinavyoendelea huko Gaza wamekamatwa.
Haijajulikana kama nyaraka hizo zina uhusiano wowote na shambulio la mtandaoni lililoilenga taasisi ya utafiti wa nyuklia ya Israel mwaka jana.


