000_42N23G2

M23 Yapinga Vikali Kuondoa Jeshi Baada ya Makubaliano

Sangiza iyi nkuru

Kikundi cha waasi cha M23 kimepinga vikali taarifa za Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa kinatakiwa kuondoa majeshi yake kutoka maeneo ya mashariki mwa nchi inayoyashikilia kwa sasa.

Jumamosi hii, M23 na serikali ya DRC walitia saini waraka unaoweka misingi ya msingi (“maadili ya msingi”), kabla ya kutiwa saini kwa makubaliano kamili ya amani kati ya pande hizo mbili.

Baada ya kutiwa saini kwa waraka huo, Waziri wa Mawasiliano na msemaji wa serikali ya DRC, Patrick Muyaya, alitangaza kuwa makubaliano hayo yanahusisha M23 kuondoa wanajeshi wake na kuruhusu vikosi vya serikali kuchukua nafasi.

Kupitia ukurasa wake wa X aliandika:
“Waraka wa misingi ya msingi tuliosaini Doha na AFC/M23 kwa upatanisho wa Qatar, unazingatia kuheshimu Katiba ya DRC, mikataba ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, maazimio ya kimataifa hasa Azimio la 2773 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na unafuata mwelekeo wa makubaliano ya Washington.”

Aliongeza:
“Makubaliano haya yanathibitisha mistari myekundu tuliyokuwa tukiitetea, hasa kutokuwepo kwa pingamizi kutoka kwa AFC/M23 katika maeneo waliyoyashikilia, yatakayochukuliwa na taasisi zetu za serikali (FARDC, Polisi ya Taifa, Mahakama, na utawala wa serikali).”

Hata hivyo, M23 kupitia kwa Katibu wake Mkuu ambaye pia alisaini waraka wa Doha, alikana taarifa hizo, akizitaja kuwa ni uongo.

Akasema:
“Hakuna sehemu yoyote katika waraka wa maadili ya msingi inayoeleza kuwa AFC/M23 inatakiwa kuondoa wanajeshi katika maeneo inayoyashikilia.”

Akaongeza:
“AFC/M23 haitarudi nyuma. Hata kwa mita moja. Tutabaki tulipo.”

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *