d0665aa0-2c50-11f0-ad09-bd0cf87606ac.jpg

Marekani: Mkimbizi wa Kongo Apigwa Risasi na Polisi – Familia Yasema Haitakata Tamaa

Sangiza iyi nkuru

Mahakama ya jimbo la Michigan imehitimisha kesi tata iliyomhusisha askari polisi aliyepigwa mshtaka kwa kumuua mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Patrick Lyoya, kwa risasi katika mji wa Grand Rapids tarehe 4 Aprili 2022.

Patrick Lyoya, aliyekuwa na umri wa miaka 26, alikimbia vita na machafuko nchini Congo akiwa na familia yake, na walihamia Marekani mwaka 2014. Baada ya kuishi Grand Rapids kwa miaka mitano, alipigwa risasi na afisa wa polisi Christopher Schurr, aliyekuwa na tajriba ya miaka saba kazini.

Video kutoka kwa kamera mbalimbali zinaonyesha Lyoya akikimbia polisi, akidungwa kwa taser, kisha kupigwa risasi akiwa chini. Polisi huyo alidai alihofia kuwa Lyoya angemdhuru au kumuua, hivyo akachukua hatua hiyo.

Kesi hiyo ilimalizika bila uamuzi, baada ya majaji kushindwa kukubaliana ikiwa afisa huyo ana hatia au la, jambo lililofanya hakimu kutangaza kuwa kesi hiyo haina mwelekeo.

Familia ya Lyoya na wafuasi wake wamesema hawatakoma kudai haki. Baba yake, Peter Lyoya, alisema: “Ni uchungu mkubwa sana. Lakini hatutakata tamaa hadi haki ipatikane kwa Patrick.”

Kifo cha Lyoya kiliibua hasira mpya miongoni mwa umma na kuibua mjadala kuhusu tabia za polisi, hasa jinsi wanavyowatendea watu weusi na wahamiaji.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *