rib-6-323af

Mhandisi wa Jiji la Kigali Akamatwa kwa Rushwa na Utakatishaji wa Pesa

Sangiza iyi nkuru

Ofisi ya Upelelezi wa Jinai nchini Rwanda (RIB) imetangaza kuwa imemkamata Ingabire Clement, ambaye ni Mhandisi Mkuu wa Ujenzi katika Jiji la Kigali.

Kupitia taarifa iliyotumwa kwenye ukurasa wao rasmi wa X, RIB ilisema kuwa Ingabire anachunguzwa kwa makosa yanayohusiana na rushwa, yakiwemo kushindwa kueleza asili ya mali aliyonayo pamoja na utakatishaji wa fedha haramu, kufuatia uchunguzi uliokuwa ukiendelea.

Mtuhumiwa huyo kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha RIB cha Nyarugenge, na jalada la kesi tayari limewasilishwa kwa Mwendesha Mashtaka.

RIB imetumia fursa hii kuonya watumishi wa umma dhidi ya kutumia madaraka yao kwa manufaa binafsi, ikisisitiza kuwa hilo ni kosa la jinai kisheria.

Aidha, ofisi hiyo imeonya umma kutoafiki mali isiyo yao kuandikishwa kwa majina yao, kwa lengo la kuwasaidia wahalifu kuficha mali walizopata kwa njia haramu, kwani nao huangukia kwenye kundi la washirika wa uhalifu.

Utakatishaji wa fedha haramu ni kosa linalopigwa marufuku chini ya Kifungu cha 23 cha Sheria Nambari 69/2018 ya tarehe 31/08/2018 kuhusu kuzuia na kuadhibu utakatishaji wa fedha na ufadhili wa ugaidi.

Adhabu yake ni kifungo cha miaka 7 hadi 10, pamoja na faini ya mara 3 hadi 5 ya thamani ya fedha iliyohusika.

Kushindwa kueleza asili ya mali ni kosa chini ya Kifungu cha 9 cha Sheria Nambari 54/2018 ya tarehe 13/08/2018 kuhusu kupambana na rushwa.

Mhusika anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 7 hadi 10, na faini ya mara 3 hadi 5 ya thamani ya mali isiyoelezwa kihalali.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *