GridArt_20250716_151856389

Paul Biya, Miaka 92, Awania Urais kwa Mara ya Nane: Je, Cameroon Yaongozwa na Wazee Pekee?

Sangiza iyi nkuru

Rais Paul Biya wa Cameroon alitangaza wiki iliyopita kuwa atawania urais kwa muhula wa nane, hatua ambayo inaweza kumfanya aongoze hadi atimize umri wa miaka 100.

Biya, mwenye umri wa miaka 92, ndiye rais mzee zaidi duniani aliye madarakani kwa sasa.

Kupitia ukurasa wake wa X, Biya alisema atagombea kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, jambo lililowashangaza wengi barani Afrika wakisema kuwa hana tena nguvu za kuongoza taifa hilo.

Upinzani umekuwa ukimtaka aondoke madarakani baada ya miaka 43 ya utawala, wakidai kuwa amepitwa na wakati.

Inadaiwa kuwa Biya huonekana mara chache hadharani na anaishi nchini Uswisi ambako amekaa kwa muda mrefu.

Mwaka jana, taarifa za kifo chake zilisambaa hadi serikali ya Cameroon ikapiga marufuku watu kujadili afya yake hadharani.

Watu wengi barani Afrika wanasema, “Jeshi la Cameroon ni wapole sana; sehemu nyingine Afrika Biya angekuwa ameondolewa madarakani zamani.”

Hata hivyo, Biya si peke yake mwenye umri mkubwa katika uongozi wa Cameroon; angalau viongozi sita wakuu ni wa kizazi chake.

Miongoni mwao ni Jenerali René Claude Meka, mwenye umri wa miaka 86, ambaye ni Mkuu wa Majeshi tangu mwaka 2001 – miaka 24 sasa.

Mkuu wa Polisi wa Cameroon, Martin Mbarga Nguélé, ana umri wa miaka 93 na amekuwa katika wadhifa huo tangu 2010. Pia ni mshauri wa rais.

Rais wa Seneti, Marcel Niat Njifenji, ana miaka 90 (karibu 91) na ameiongoza tangu 2013.

Spika wa Bunge, Cavayé Yeguié Djibril, ana miaka 85 na amekuwa kwenye nafasi hiyo tangu 2012.

Waziri wa Sheria, Laurent Esso, ana miaka 83 na amehudumu tangu Desemba 2011.

Rais wa Mahakama ya Katiba, Clément Atangana, ana miaka 84 na amekuwa kwenye nafasi hiyo tangu 2018.

  • Martin Mbarga Nguélé, miaka 93 – Mkuu wa Polisism 1698483919.450633

  • Marcel Niat Njifenji, miaka 90 – Rais wa Seneti000 32MY36U

  • Laurent Esso, miaka 83 – Waziri wa Sheriajad20241231 ass cameroun evacuation sanitaire laurentesso

  • Cavayé Yeguié Djibril, miaka 85 – Spika wa Bungejad20250429 ss cavaye yeguie

  • Clément Atangana, miaka 84 – Rais wa Mahakama ya KatibaIMG 20241109 093843 227

  • Paul Biya, miaka 92 – Anawania tena OktobaScreenshot 2024 10 08 214133

  • Jenerali René Claude Meka, miaka 86 – Mkuu wa Jeshi tangu 2001Screenshot 20250716

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *