portrait-sensitive-man-crying-weeping-black-man-1280px-t-750x375

Taharuki Zimbabwe! Mwanamke Akamatwa kwa Kumlazimisha Ex Wake Kufanya Ngono Bila Kinga ili “Kuvunja Uchawi”

Sangiza iyi nkuru

Polisi wa Harare, Zimbabwe wamemkamata Amanda Chizanga Chakanyuka, mwenye umri wa miaka 26, kwa tuhuma za kumteka aliyekuwa mpenzi wake, Linos Gapanga, 38, na kumlazimisha kufanya ngono bila kinga, akidai ni kwa ajili ya kuondoa uchawi.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Zimbabwe, Amanda alikwenda nyumbani kwa Linos katika eneo la Glen View, siku ya Jumamosi, 12 Julai 2025, akiwa na wanaume watano wasiojulikana. Walimkamata na kumpeleka kwenye nyumba ya kulala wageni ya Machipisa Pink Lodge.

Gapanga alisema alipigwa, kisha kufungiwa kwenye chumba na Amanda, na kulazimishwa kufanya naye ngono. Baada ya tukio hilo, walimnyang’anya dola 142 na kadi za benki.

Polisi wamethibitisha kukamatwa kwa Amanda, lakini wanaume watano bado wanasakwa. Mhasiriwa alipelekwa katika Hospitali ya Sally Mugabe, akiwa na majeraha usoni na ubavuni, na sasa anataka haki.

Kisa hiki kimezua mjadala mkubwa mitandaoni, wengi wakikiona kama unajisi wa kingono unaochochewa na imani za kishirikina.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *