M23

Walikale: M23 Yawashinda Wazalendo, Yachoma Kambi Zao

Sangiza iyi nkuru

Kikundi cha waasi wa M23 kimewafurusha wapiganaji wa vikundi vya kijeshi vya Wazalendo kutoka kijiji cha Mulema, katika eneo la Kisimba, Wilaya ya Walikale, baada ya kuwashinda katika mapigano.

Mapigano makali yalizuka kati ya pande hizo mbili siku ya Jumapili, tarehe 8 Juni.

Ripoti zinaeleza kuwa wapiganaji wa M23 waliokuwa wakitokea eneo la Kalonge walishambulia kambi za Wazalendo zilizokuwa Mulema, kabla ya kuteka eneo hilo.

Baada ya wapiganaji wa Wazalendo kutoroka, M23 inasemekana walichoma moto kambi zao pamoja na maeneo mengine kabla ya kuondoka.

M23 imekuwa ikidhibiti sehemu za eneo la Kisimba tangu Februari mwaka huu walipoingia katika Wilaya ya Walikale.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *