Mahakama ya Msingi Mjini Kigali imeamua kumuacha huru kwa dhamana aliyekuwa Waziri wa Utamaduni na Michezo, Robert Bayigamba.
Bayigamba alikamatwa tarehe 22 Octoba juu ya tuhuma za kununua mali za watu kinyume na sheria.
Mahakama imesema hakuna sababu maaalumu zinazeweza kumfanya Bayigamba aendelee kufungwa.
Upande wa mwendeshamashtaka umepewa siku tano kupiga rufaa ya uamuzi huo.
Mahakamani, Bayigamba alisema haiwezekani yeye kutoroka kwani ni mtu maarufu nchini.
Bayigamba ni mwenyeji wa kiwanda cha Manumetali ambacho thamani yake ni Frw bilioni tatu.
Aliongoza kampuni kadhalika nchini Rwanda kama vile RwandAir, na SORAS.
Isangize abandi
Tanga igitekerezo