Maeneo kadhaa katika Wilaya ya Walikale, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), yamerejea mikononi mwa waasi wa AFC/M23. Ripoti zinaonyesha hata kituo kikuu cha mji wa Walikale, ambacho awali walikiondoka baada ya mazungumzo ya Doha, kimechukuliwa tena.
Mashuhuda wa eneo hilo wamethibitisha kuwa wapiganaji wa AFC/M23 walianzisha mashambulizi mapya kuchukua Walikale. Mapigano makali kati yao na jeshi la Congo (FARDC) pamoja na wapiganaji wa Wazalendo yaliendelea kwa siku nzima Jumanne iliyopita.

Hali hii imetokea baada ya kuvunjika kwa mazungumzo ya amani ya Doha, kufuatia serikali ya Kinshasa kukataa kuwaachilia wafungwa wa kisiasa na wanajeshi wa AFC/M23 kama ilivyokuwa imepangwa.
AFC/M23 walikabidhi orodha ya zaidi ya wafungwa 700 wanaodaiwa kushikiliwa kinyume cha sheria na serikali ya Congo, wengi wao wakiwa walikamatwa kwa tuhuma za kuhusiana na Christophe Baseane Nangaa, aliyekuwa Gavana wa Haut-Uélé.


