72316079_905

Vatikani: Mwili wa Papa Francis Wafikishwa Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro

Sangiza iyi nkuru

Mwili wa Papa Francis umefikishwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatikani ili kupewa heshima za mwisho kabla ya kuzikwa Jumamosi ijayo. Zaidi ya watu 20,000 walijitokeza katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kumuaga.

Asubuhi ya Jumatano, jeneza lake lililokuwa wazi lilibebwa kutoka katika chapel ya Casa Santa Marta, alipofariki. Safari hiyo iliandamana na makadinali waliovaa mavazi mekundu na walinzi wa Papa wa Uswisi waliovaa mavazi yao ya rangi ya dhahabu, njano na buluu.

Kardinali Kevin Farrell aliongoza shughuli hiyo. Yeye ndiye atakayeongoza shughuli za Vatikani kwa muda hadi Papa mpya atakapochaguliwa, kuchukua nafasi ya Papa Francis aliyefariki Jumatatu tarehe 21 Aprili 2025.

Papa Francis, aliyezaliwa kwa jina Jorge Mario Bergoglio huko Flores, Buenos Aires nchini Argentina tarehe 17 Desemba 1936, aliongoza Kanisa Katoliki tangu 2013 baada ya kujiuzulu kwa Papa Benedict XVI.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *