7386c370-2592-11f0-9aa5-b1af329323e6.jpg

Alifanyiwa Upasuaji Zaidi ya Mara 100 Kutafuta Uzuri… Lakini Bado Anajiona Mbaya

Sangiza iyi nkuru

Abby Wu, msichana wa Kichina aliyekuwa na miaka 14 tu alipofanyiwa upasuaji wake wa kwanza, alitaka kubadilisha mwili wake ili awe mzuri zaidi. Sasa akiwa na miaka 35, tayari amefanyiwa upasuaji zaidi ya mara 100, akitumia karibu nusu milioni ya dola za Kimarekani.

Wakati wasichana wengine wa rika lake walikuwa wakifikiria kuhusu masomo au michezo, Abby alianza safari ya kutafuta “uzuri wa kipekee”. Ilianza baada ya kukosolewa na mwalimu wake wa dansi aliyemwambia kwamba alikuwa na unene kupita kiasi, akimtaka achague kati ya kupunguza uzito au kuacha kucheza dansi. Mama yake alimpeleka hospitali kufanyiwa liposuction (kutoa mafuta mwilini).

Hospitalini, Abby alipatiwa dawa ya usingizi wa maumivu lakini hakulala. Aliona kila kitu kilichokuwa kikifanyika, hata damu ikitiririka. Upasuaji huo wa kwanza ukawa mwanzo wa hadithi ya kushangaza na ya maumivu.

Kwa sasa, Abby anamiliki kliniki ya urembo katikati ya Beijing na anajulikana kama mmoja wa wanawake waliowahi kufanyiwa upasuaji mara nyingi zaidi nchini China. Kupitia mtandao wa kijamii wa SoYoung unaohusu huduma za urembo, Abby hushirikisha watu safari yake ya upasuaji. Hata baada ya kufanyiwa upasuaji mara nyingi, programu ya uchunguzi wa urembo iitwayo “Magic Mirror” bado inaonyesha kasoro kwenye uso wake, hali inayomlazimisha kupanga upasuaji mwingine.

Nchini China, watu milioni 20 hufanyiwa upasuaji wa urembo kila mwaka, wengi wao wakiwa wasichana walio na umri chini ya miaka 25. Wengi huenda kwenye vituo visivyo na leseni, hali ambayo mara nyingi husababisha vilema au kifo.

Yue Yue, msichana wa miaka 28, alikuwa mmoja wa waathirika wa upasuaji mbaya. Alidungwa dawa ili kumpa sura ya mtoto, lakini uso wake ukaishia kufanana na saruji. Alifanyiwa upasuaji wa kuondoa dawa hiyo kwa maumivu makali na kubaki na ulemavu wa kudumu.

Mnamo mwaka 2020, mwigizaji Gao Liu naye alipata madhara baada ya upasuaji wa pua uliosababisha pua yake kuoza. Tukio hilo liliwashangaza watu wengi nchini China na kuonyesha ukubwa wa tatizo la vituo vya upasuaji visivyo na kibali.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *