Baada ya kutokuelewana katika uongozi wa timu ya Inter Star, ambapo baadhi ya viongozi walipinga kuuza timu yao, wachezaji Nyange na Caleb waliamua kubadili mwelekeo wao.
Wachezaji hawa wawili walikuwa wameungana katika mradi wa kuinunua Inter Star, lakini mpango huo uligonga mwamba kutokana na msimamo wa viongozi waliotaka timu isiuzwe bali ipate msaada wa kifedha.
Baada ya kujadiliana upya, Nyange na Caleb waliamua kununua timu ya Royal Vision 2026, badala ya kuendelea kusisitiza kuhusu mradi wa Inter Star.
Hadi sasa, haijajulikana Inter Star itatatua vipi matatizo yake ya kifedha, huku Royal Vision 2026 ikianza safari mpya chini ya uongozi wa wachezaji hao wawili.


