iran-israel-28-ap-gmh-250613_1749843098733_hpMain_16x9

Iran Yarushia Israel Mvua ya Makombora kwa Kisasi Kikali

Sangiza iyi nkuru

Usiku uliopita, Iran ilirusha makombora mengi kuelekea Israel, kama kisasi kwa mashambulizi makali ambayo Israel iliifanya dhidi yake mapema asubuhi ya Ijumaa.

Mashambulizi ya Israel yalileta madhara makubwa kwa Iran, yakiangamiza miundombinu muhimu ya kutengeneza silaha za nyuklia na kuwaua viongozi wakuu wa kijeshi pamoja na wanasayansi mashuhuri wa Iran.

Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa alitangaza kuwa watu 78 waliuawa na wengine takribani 320 walijeruhiwa.

Kwa kulipiza kisasi, jioni ya Ijumaa Iran ilirusha makombora ya masafa marefu (ballistic missiles) katika maeneo mbalimbali ya Israel.

Video zilizosambazwa mitandaoni zilionyesha makombora mengi ya Iran yakilenga miji ya Tel Aviv na Yerusalemu, ambapo milipuko mikubwa ilisikika.

Makombora hayo yalirushwa kwa awamu tofauti, na yalifuata shambulio la awali la drone za kujitoa mhanga kutoka Iran dhidi ya Israel siku ya Ijumaa.

Hadi sasa, ni vigumu kujua hasara kamili iliyosababishwa na mashambulizi hayo ya Iran.

Ripoti za awali zinaonyesha kuwa Waisraeli 40 wamejeruhiwa, wakiwemo wawili walioumia vibaya na wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini.

Balozi wa Israel nchini Marekani alithibitisha kuwa mwanamke mmoja alifariki kutokana na mashambulizi hayo.

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) kupitia ukurasa wao wa X lilisema kuwa walikuwa wakifanya “uteketezaji wa makombora pale inapohitajika”, ili kuzuia athari zaidi.

IDF pia iliwaonya Waisraeli kuwa Iran inaweza kufanya mashambulizi zaidi, na kuwataka wakae karibu na maeneo salama.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, aliwataka Iran na Israel kusitisha mzozo na kukubaliana na usitishaji wa mapigano.

Kupitia ukurasa wake wa X, aliandika: “Israel yashambulia maeneo ya nyuklia ya Iran, Iran yajibu kwa makombora Tel Aviv. Tension imezidi. Ni wakati wa kusitisha. Amani na diplomasia ndiyo suluhisho.”

Viongozi wa nchi za Magharibi wakiongozwa na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Donald Trump wa Marekani, walisema kuwa Israel ina haki ya kujilinda inapohisi usalama wake unatishiwa na Iran.

Kwa upande mwingine, nchi nyingi za Asia zikiongozwa na Pakistan, zilikemea vikali mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran na kuonya kuwa Israel italazimika kulipia gharama hizo.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *