20250614_074418

Rais Samia Aingilia Kati, Mechi ya Yanga na Simba Hatimaye Kufanyika

Sangiza iyi nkuru

Vilabu vya Tanzania Young Africans (Yanga) na Simba Sports Club hatimaye vimekubaliana kucheza mechi yao ya ligi, baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati mgogoro uliokuwepo.

Awali, timu hizo zilipaswa kukutana tarehe 8 Machi, lakini mechi haikufanyika baada ya Simba kugoma kucheza, wakidai kunyimwa nafasi ya kufanya mazoezi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na mashabiki wa Yanga waliopaswa kuwa wenyeji wa mechi hiyo.

Mazoezi hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika saa 24 kabla ya mechi.

Baada ya mechi hiyo kufutwa, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliipanga tarehe nyingine; hata hivyo, Yanga walikataa kabisa kucheza, wakisisitiza kuwa Simba wapewe adhabu ya kufungiwa, na wao wapewe alama tatu.

Mgogoro huo ulipelekea hata Waziri wa Michezo wa Tanzania kuingilia kati akihimiza timu zote mbili zikubali kucheza, lakini juhudi hizo hazikufanikiwa.

Kesi hiyo iliwasilishwa pia katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) na Mahakama Kuu ya Tanzania, lakini mahakama zote mbili zilipinga maombi ya Yanga. Mahakama Kuu iliamuru mechi ichezwe tarehe 15 Juni, siku ya Jumapili, lakini Yanga walikataa amri hiyo vikali.

Baada ya miezi mitatu ya mvutano mkali, ilibidi Rais Samia Suluhu Hassan aitwe viongozi wa timu hizo ofisini kwake Ijumaa, tarehe 13 Juni, kwa lengo la kumaliza mvutano huo unaozidi kutokota.

Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Rais Samia alisema mazungumzo na viongozi hao yalilenga maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania.

Mazungumzo hayo yalimalizika kwa Simba na Yanga kukubaliana kwamba mechi hiyo ichezwe tarehe 25 Juni mwaka huu.

Zikiwa zimebaki mechi tatu kufikia mwisho wa Ligi Kuu Tanzania, Yanga inaongoza kwa pointi 73, ikiwa mbele ya Simba yenye pointi 72.

Hii ina maana kuwa mshindi wa mechi hiyo ndiye atakayekuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi ya msimu huu.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *