Mchezaji nyota wa Real Madrid, Kylian Mbappé, amekimbizwa hospitalini kutokana na ugonjwa wa tumbo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo siku ya Alhamisi.
Mbappé hakushiriki mechi ya kwanza ya timu yake kwenye michuano ya Kombe la Dunia la Klabu, iliyofanyika Miami dhidi ya Al Hilal ya Saudi Arabia siku ya Jumatano, kutokana na homa kali.
Kocha wa Real Madrid, Xabi Alonso, alisema ana matumaini kuwa Mbappé atakuwa amepona kabla ya mechi inayofuata siku ya Jumapili dhidi ya Pachuca.
Klabu imesema kuwa Mbappé atafanyiwa vipimo mbalimbali vya afya na atafuatiliwa kwa karibu na madaktari.
Kutokuwepo kwa Mbappé ni pigo kubwa kwa mashindano haya, hasa kwa kuwa yeye ni mmoja wa wachezaji bora duniani.
FIFA, ambayo ndiyo inasimamia mashindano haya, inalenga kuyafanya kuwa ya hadhi ya juu na yanayovutia mashabiki wengi duniani kote.


