Rais wa Marekani, Donald Trump, amekataa ombi la Rais wa Urusi, Vladimir Putin, la kumsaidia kuanzisha mazungumzo na Iran ili kupunguza mvutano kati ya Iran na Israeli.
Katika mahojiano na Fox News, Trump alisema kuwa Putin alimpigia simu na kumwahidi kuwa anaweza kusaidia kutafuta amani, lakini Trump alimjibu: “Sina shida na Iran, shida yangu ni wewe.”
Trump alisisitiza kuwa hakuna mazungumzo yoyote ya upatanisho yanaweza kufanyika wakati Urusi inaendelea na vita nchini Ukraine, akisema kuwa zaidi ya wanajeshi elfu sita waliuawa wiki iliyopita.
Wachambuzi wa kimataifa wanaona kuwa Putin anajaribu kuonyesha kuwa Urusi inaweza kuwa mpatanishi wa amani, lakini kwa upande wake Trump alisema anachotaka ni Urusi kusitisha vita kabla ya kuzungumzia ushirikiano wowote.
Trump pia alizungumzia kuhusu hali ya tahadhari iliyovunjika kati ya Iran na Israeli baada ya Israeli kuripoti kwamba Iran imeanza tena kurusha makombora. Hii ilimfanya Trump kusema: “Nchi hizi mbili zinaleta maumivu ya kichwa,” huku akionyesha kutoridhishwa na mwenendo wa Israeli.


