Hakimu wa Kigali akamatwa kwa kughushi

Sangiza iyi nkuru

Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda (RIB) imemkamata hakimu wa Mahakama ya kati ya Nyarugenge, Eric Twambajimana kwa kughushi nyaraka .

Kwa mujibu wa chombo hicho cha uchunguzi, Twambajimana aliwekwa kizuizini baada ya kutoa karatasi bandia za wito wa RIB kwa mtu ambaye ametoroka nchini hivyo anaweza kuzitumia kutafuta hifadhi katika nchi ya Ulaya akihoji kuwa anatafutwa na RIB kwa sababu za kisiasa.

Mshukiwa anazuiliwa katika kituo cha Kacyiru RIB, mjini Kigali, huku uchunguzi ukiendelea.

Ofisi hiyo pia ilifichua kuwa hati ghushi zilikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali.

Akipatikana na hatia, Twambajimana anaweza kufungwa jela miaka saba na faini ya hadi milioni 5 .

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *