Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema Finland itajiunga na muungano wa kijeshi siku ya Jumanne, chini ya mwaka mmoja baada ya nchi hiyo kuwasilisha ombi lake kujibu uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine .
Stoltenberg aliwaambia waandishi wa habari kabla ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa NATO kwamba Finland inaleta jeshi lililofunzwa vyema na lenye vifaa vya kutosha katika muungano huo baada ya Uturuki kuwa mwanachama wa mwisho wa kutoa kibali chake katika mchakato ambao lazima uwe kwa kauli moja.
Stoltenberg pia alisema “ana imani kabisa” kwamba Uswidi itaifuata Ufini kama mwanachama mpya wa NATO, na kwamba ni kipaumbele kwa hilo kutokea haraka iwezekanavyo.
Uturuki imepinga ombi hilo la Uswidi, hasa kutokana na kile ambacho Ankara inasema ni Uswidi kuwa mpole sana kwa makundi ambayo Uturuki inayachukulia kuwa ni magaidi. Stoltenberg alisema anaamini Sweden imetimiza hatua ilizokubali katika mazungumzo na Uturuki ili kuondoa wasiwasi huo.


