AtlanticCouncil

Mazungumzo ya Iran na Marekani Yavunjika Oman Baada ya Shambulizi Kubwa la Israel

Sangiza iyi nkuru

Jumamosi iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Badr Albusaidi, alitangaza kuwa awamu ya mwisho ya mazungumzo kuhusu silaha za nyuklia kati ya Marekani na Iran yaliyopangwa kufanyika Jumapili mjini Muscat hayataendelea tena. Oman imekuwa mpatanishi wa muda mrefu katika mazungumzo haya.

Albusaidi alitoa tangazo hilo siku moja baada ya Israel kufanya shambulio kubwa dhidi ya Iran, likiwalenga na kuwaua maafisa wa kijeshi wa ngazi za juu pamoja na wataalamu wa silaha za nyuklia. Pia ilishambulia maeneo yanayodhaniwa kuwa yanatengeneza silaha hizo kwa lengo la kuzuia Iran kumiliki silaha za nyuklia.

Afisa mwandamizi katika serikali ya Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alithibitisha kuwa kikao cha Jumapili kimesitishwa rasmi.

Wakati huo huo, hali ya mvutano kati ya Israel na Iran inaendelea kuwa mbaya zaidi, huku pande zote zikizindana makombora na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (drones). Shambulizi la Iran karibu na Haifa na Tel Aviv liliripotiwa kuua watu 10 na kujeruhi zaidi ya 100.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *