99303709-14806255-image-a-1_1749736347217

Nabii wa Kihindi Alitabiri Ajali ya Ndege ya Air India ya 2025

Sangiza iyi nkuru

Nabii kutoka India aitwaye Astro Sharmistha anaripotiwa kuwa alitabiri kwa muda mrefu janga kubwa la ajali ya ndege katika mwaka wa 2025, kabla ya ajali ya hivi karibuni ya ndege ya Air India iliyogharimu maisha ya watu wengi.

Nabii huyo aliwaambia wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii kwamba “mwaka 2025 utaleta habari za kuhuzunisha kuhusu ajali za ndege.” Wiki iliyopita, alikumbusha tena kwamba unabii wake unaweza kutimia hivi karibuni.

Ajali hiyo ilitokea Alhamisi asubuhi, wakati ndege aina ya Boeing 787 Dreamliner iliyokuwa ikitoka Ahmedabad kuelekea London ilianguka dakika chache tu baada ya kupaa.

Ndege hiyo ilikuwa na abiria 242, wakiwemo Wazungu 53, Wahindi 159, Wareno saba, Mkanada mmoja, pamoja na watoto 11 wakiwemo watoto wachanga wawili. Hadi sasa, vikosi vya uokoaji kwa kushirikiana na jeshi vimefanikiwa kuokoa miili 204 kutoka eneo la ajali, huku wengine wengi wakiendelea kutafutwa.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *