Agakarita-ko-gushyiraho-amafaranga-yamazi-akajya-yishyurwa-mbere-ukojeje-ku-kamashini-kabugenewe-768x576

Rwanda Kuanza Mfumo wa Malipo ya Maji kwa Njia ya Kadi Kama Umeme

Sangiza iyi nkuru

Mkurugenzi Mkuu wa WASAC, Prof. Omar Munyaneza, ametangaza kuwa mfumo mpya wa malipo ya maji kabla ya matumizi (prepaid), kama ule wa umeme, unatarajiwa kuanzishwa. Teknolojia hii itasambazwa kote nchini baada ya majaribio kufanyika kwenye visima vya maji vya umma katika wilaya za Rwamagana, Kayonza, Gatsibo na Nyagatare.

Katika mfumo huu, watu wataweka pesa kwenye kadi ambayo wataipitisha kwenye mashine iliyowekwa kwenye bomba la maji, na hivyo kupata kiasi cha maji kulingana na pesa walizolipia.

“Mwananchi atatumia kifaa kidogo kinachofanana na sarafu inayoitwa ‘token’, au kama kadi ya Tap&Go. Ataenda kwenye bomba, akiweka token ya Rwf 100, na kama galoni moja ni Rwf 20, hiyo kiasi itakatwa. Kesho akirudi, ataongeza tena mpaka salio lake liishe, kisha aweke nyingine,” Prof. Omar alieleza siku ya Jumatano.

Alisema kuwa majaribio kwenye visima 200 vya maji vya umma yalifanikiwa, na sasa mfumo huo uko tayari kuanza kutekelezwa nchi nzima huku wakandarasi wakiwa tayari wamepatikana.

Aliongeza: “Kama vile mnavyonunua umeme kwa kutumia cash power, ndivyo tunavyotaka kufanya kwa maji. Tumeshaweka tangazo kwa wale wanaotaka kushirikiana na WASAC, na wengine wenu mtawaona mafundi wakifunga mfumo huu majumbani kwenu hivi karibuni.”

Prof. Omar alisisitiza kuwa mfumo huo utasaidia wananchi kujitunzia matumizi yao ya maji, kuondoa malalamiko ya bili zisizo sahihi, na pia kurahisisha ukusanyaji wa malipo kwa WASAC.

Alisema pia kwamba endapo mfumo huo utafanikiwa ndani ya miezi sita ijayo, utaenezwa kote nchini.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *