IWI X95 (zamani ikiitwa Micro-Tavor, MTAR au MTAR-21) ni bunduki iliyoundwa na kutengenezwa na kampuni ya Israel Weapon Industries (IWI), sehemu ya familia ya bunduki ya Tavor, ikijumuisha Tavor TAR na Tavor 7. Sasa hivi, bunduki hii inatengenezwa pia nchini Rwanda kupitia kampuni ya Remico, kwa ushirikiano na IWI.

Kitengo cha kupambana na ugaidi (CTU) cha Rwanda ni miongoni mwa vikosi vinavyotumia Tavor X95.
Historia
Mnamo Novemba 2009, X95 ilichaguliwa kuwa bunduki ya kizazi kipya kwa Jeshi la ardhini la Israeli.

Mpaka sasa, ni mojawapo ya bunduki tatu za kisasa zinazotumika rasmi na Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF). Pia hutumiwa na Jeshi la Rwanda, hasa na walinzi wa Rais na kitengo maalum cha kupambana na ugaidi (CTU).
Katika India, wakati wa mapambano dhidi ya waasi huko Kashmir, makamanda wa CRPF waliripoti kwamba X95 ni bora zaidi ya AKM, kwa sababu ya urefu mfupi, nguvu kubwa, usahihi wa mbali na uzito mdogo.

Jeshi la Azerbaijan pia hutumia Tavor X95.
Mnamo 2014, IDF ilitangaza mipango ya kuongeza uwezo wa baadhi ya bunduki za X95, ikiwa ni pamoja na kuongeza urefu wa pipa hadi 380 mm, kutoka 330 mm ya awali, na kuongeza trigger nyepesi.
Mnamo Septemba 2021, iliripotiwa kuwa vikosi vya mstari wa mbele vya Israeli vilianza kubadilisha bunduki za Micro Tavor na M4, huku zile za zamani zikihamishiwa kwa brigedi za akiba.

Rwanda yajitosa katika utengenezaji wa silaha
Hivi karibuni, Rwanda ilitangaza kwa dunia kuwa sasa inatengeneza silaha zake, ikiwa ni pamoja na bunduki ya Tavor X95.
Tarehe 7 Septemba, tovuti ya Kiyahudi ya IDF iliripoti kuwa jeshi la Israeli limepanga kuendelea kutumia Micro Tavor na kuzipatia vikosi vya mapambano.
X95 inatofautishwa na TAR-21, CTAR-21, STAR-21 na GTAR-21 kwa muundo wake wa kipekee.

Mataifa yanayotumia Tavor X95
Bunduki za Tavor X95 zinazotengenezwa Kigali zinatumiwa si tu na Rwanda na Israeli, bali pia na mataifa kama:
Marekani, Azerbaijan (ambapo Rais Kagame alitembelea majuzi), Morocco, Colombia, Senegal, Thailand, Ukraine, Philippines, Honduras, India, Indonesia, Angola, Georgia, na mengine.


