urnpublicidap.org889e2ba4274ec2de030e0fcf15cf81d6Musk_Trump_00091

Trump Amshambulia Elon Musk kwa Kuanzisha “America Party”

Sangiza iyi nkuru

Rais wa Marekani Donald Trump alishambulia vikali Elon Musk, aliyekuwa mshauri wake na tajiri namba moja duniani, siku ya Jumapili baada ya kutangaza kuanzisha chama kipya cha siasa kitakachopinga vyama viwili vikuu vya kisiasa.

Katika mahojiano mafupi na waandishi wa habari kabla ya kupanda ndege ya rais, Air Force One, Trump alisema:

“Nafikiri kuanzisha chama cha tatu ni upumbavu. Tangu zamani tumekuwa na mfumo wa vyama viwili, na kuanzisha chama cha tatu kutazidisha tu mkanganyiko.”

Kauli hiyo ilikuja siku moja tu baada ya Musk kutangaza kupitia mtandao wake wa kijamii X kwamba ameanzisha chama kipya kiitwacho America Party, ili kuleta ushindani dhidi ya vyama vya Republican na Democrat.

Elon Musk, anayemiliki kampuni kubwa kama Tesla, mtengenezaji wa magari yanayotumia umeme, alikuwa amepewa uongozi wa wizara mpya iitwayo DOGE (kifupi cha Kiingereza), iliyoanzishwa kusaidia kupunguza matumizi ya serikali. Baadaye aligombana na Trump baada ya kutofautiana kuhusu sheria ya kodi iliyoathiri maslahi yake.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *