trump-iran

Trump Aonya: “Marekani Inaweza Kuirushia Iran – Watu Wote Waondoke Tehran Sasa”

Sangiza iyi nkuru

Rais wa Marekani, Donald Trump, amewataka watu wote kuondoka mji mkuu wa Iran, Tehran, kufuatia tetesi kwamba shambulizi linaweza kutokea muda si mrefu.

Trump alitoa ujumbe huo kupitia mtandao wake wa Truth Social, akisema:

“Iran ilipaswa kukubali makubaliano niliyopendekeza. Inasikitisha kuona maisha mengi yakipotea. Iran haipaswi kamwe kumiliki silaha za nyuklia. Nimerudia mara nyingi. Wote walioko Tehran wanapaswa kuondoka sasa hivi.”

Baada ya tangazo hilo, Israeli nayo ilitoa tamko kama hilo, ikiwataka raia wake kuondoka katika baadhi ya maeneo ya Tehran, huku mvutano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili ukizidi kuongezeka.

Iran ilijibu kwa kusema kwamba huu ni ushambulizi wa kisaikolojia unaolenga kutisha raia wake.

Viongozi wa mataifa ya G7 walitoa tamko la pamoja wakisisitiza haki ya Israeli kujilinda, na kumlaumu Iran kwa kusababisha hali ya kutokuwa na usalama katika eneo hilo.

Walitoa wito wa kutafuta suluhisho la amani, likijumuisha kusitishwa kwa vita Gaza, ili kurejesha utulivu Mashariki ya Kati.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *