Wanaume wawili waliokuwa wakirusha maudhui kwenye chaneli ya YouTube Dawa Rwanda TV wamekamatwa na Ofisi ya Upelelezi wa Jinai ya Rwanda (RIB) wakishutumiwa kwa kusambaza taarifa za uongo na kutumia lugha inayochochea mfarakano miongoni mwa raia.
RIB ilitangaza kuwa kukamatwa kwao kulifanyika kwa ushirikiano na Polisi ya Taifa ya Rwanda mnamo tarehe 10 Juni 2025, na kwamba kwa sasa wanazuiliwa katika Kituo cha RIB cha Remera huku uchunguzi ukiendelea.
Msemaji wa RIB, Dkt. Thierry B. Murangira, alisisitiza kuwa mitandao ya kijamii inapaswa kutumiwa kwa manufaa ya kijamii, na akawakumbusha wananchi kwamba kuvunjilia mbali umoja wa kitaifa kupitia mitandao ni kosa la jinai linaloadhibiwa kwa mujibu wa sheria.


