Tarehe 21 Aprili 1994, wakati mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi yalipokuwa kwenye kilele, ndio siku ambayo idadi kubwa zaidi ya Watutsi waliuawa nchini Rwanda.
Katika maeneo mbalimbali ya nchi, zaidi ya Watusi 250,000 waliuawa katika maeneo tofauti kama vile Murambi, Cyanika, Nyanza, Kinazi, Cyarwa-Tumba, na mengineyo.
Utafiti wa MINUBUMWE (Wizara ya Umoja wa Kitaifa na Uhamasishaji wa Kiraia) unaonyesha kuwa tarehe 21 Aprili 1994 ndiyo siku ya mauaji ya watu wengi zaidi kwa mpigo katika historia ya mauaji hayo.
Kwa mujibu wa utafiti:
-
Watu zaidi ya 50,000 waliuawa Murambi (Nyamagabe, zamani Gikongoro),
-
Zaidi ya 35,000 waliuawa katika Parokia ya Cyanika, Nyamagabe,
-
Takribani 47,000 waliuawa katika Parokia ya Kaduha, pia Nyamagabe.
Serikali ya mauaji iliendelea kununua silaha na kugawa fedha kwa wananchi ili kuchochea mauaji.
MINUBUMWE inasema kuwa kupitia sera ya “ulinzi wa kiraia”, serikali iliwaingiza raia wa Kihutu katika mauaji, ikiwapatia silaha na fedha ili kuhakikisha Watutsi wanamalizwa kabla majeshi ya FPR hayajafika.
Wakati serikali ya mauaji ilikuwa ikishindwa vitani, iliharakisha mauaji kwa kuwapa mawaziri majukumu ya kuangalia maeneo maalum.
Miongoni mwa waliohusika:
-
Pauline Nyiramasuhuko – Butare,
-
Edouard Karemera na Eliezer Niyitegeka – Kibuye,
-
Callixte Nzabonimana – Gitarama,
-
Augustin Ngirabatware – Gisenyi.
Kamati ziliundwa kuficha ushahidi kwa kubomoa nyumba na kuondoa miili ya waliouawa.
Siku hiyo, vikundi vikubwa vya Wahutu waliokuwa na silaha waliingia maeneo ya wakimbizi wa Kiwatusi. Saa tatu asubuhi, Interahamwe waliovaa majani ya ndizi waliwashambulia wakimbizi kutoka pande zote na kuwaua.
Watoto waliosalimika walilishwa uji uliowekwa tindikali na waliuawa.
Miili ya takribani watu 70,000 ilizikwa kwenye Ukumbusho wa Mauaji ya Kimbari wa Karama.
Tarehe hiyo hiyo, Watutsi waliuawa Gishubi, wakiwemo wakazi na waliokuwa wakikimbia kutoka Ndora, Musha, na Gikongoro.


