Untitled-1

Tension Yazidi: Wahouthi Wafyetua Kombora la Ballistic kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ben Gurion, Israel

Sangiza iyi nkuru

Kombora la ballistic lililorushwa kutoka Yemen limeanguka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ben Gurion nchini Israel, na kusababisha uharibifu wa barabara na magari, huku safari za ndege zikisitishwa kwa muda, kama inavyoonyeshwa na picha na video zilizothibitishwa na Al Jazeera.

Jeshi la Israel limethibitisha kuwa mifumo yao ya ulinzi haikufanikiwa kuzuia kombora hilo mapema asubuhi ya Jumapili, licha ya juhudi zilizofanyika. Uchunguzi unaendelea na huduma za uokoaji zimeripoti kuwa watu wanane wamejeruhiwa.

Waasi wa Houthi kutoka Yemen, ambao wameongeza mashambulizi dhidi ya Israel wakisema ni njia ya kupinga vita vyao huko Gaza, wamethibitisha kuwa wao ndio waliofyatua kombora hilo lililolenga uwanja huo wa ndege unaopokea abiria wengi zaidi nchini humo.

Kwa mujibu wa viongozi wa Palestina, mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza katika kipindi cha miezi 18 yaliyopita yamesababisha vifo vya watu 52,495, wakiwemo 57 waliokufa kwa njaa kutokana na mzingiro wa Israel uliowekwa tangu Machi 2.

Katika hotuba ya televisheni, msemaji wa kijeshi wa Wahouthi, Yahya Saree, alitoa onyo kwa mashirika ya ndege, akisema kuwa Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion hauko salama tena kwa safari za anga.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *