77c31627-bf4a-47f2-a925-4d1e0e6690ee

Kenya: Polisi Wakamatwa Watu Wanne Kwa Mauaji ya Mbunge Charles Ong’ondo Were

Sangiza iyi nkuru

Jeshi la Polisi la Kitaifa la Kenya (NPS) limetangaza kukamatwa kwa watu wanne wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya Mbunge wa Kasipul, Charles Ong’ondo Were.

Katika taarifa za hivi punde, polisi wamesema kwamba wachunguzi walibaini kuwapo kwa watu hao wanne katika eneo la tukio na pia walikusanya ushahidi muhimu wa kuwahusisha na mauaji hayo.

“Baada ya kuchambua ushahidi zaidi uliokusanywa awali, maafisa wa polisi wa ofisi ya kitaifa walitekeleza oparesheni na kuwakamata washukiwa wanne waliobainika kuwa kwenye eneo la tukio la uhalifu,” alisema Msemaji wa Polisi, Muchiri Nyaga.

Aliendelea kusema kuwa wachunguzi pia walipata ushahidi muhimu unaohusiana moja kwa moja na tukio hilo pamoja na watuhumiwa wake.

Kwa mujibu wa gazeti la The Star nchini Kenya, baadhi ya watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa wanachama wa magenge hatari ya kihalifu yanayoendesha shughuli zao katika eneo la Eastlands, kusini mashariki mwa Nairobi.

“Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa ni wanachama wa magenge ya kihalifu yaliyo na mpangilio maalum kama vile ‘Mjahidin’ ambalo linajihusisha na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha katika eneo la Eastlands,” aliongeza Nyaga.

Polisi wamewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu na kujiepusha na uvumi, wakisisitiza kuwa uchunguzi wa kina unaoendeshwa kwa umakini na bila upendeleo unaendelea.

Aidha, mamlaka zimewaomba watu wasiokuwa sehemu ya uchunguzi huo kuepuka kutoa maoni au taarifa zinazoweza kuvuruga juhudi za kuwaweka wahusika wa mauaji ya Mbunge Were mikononi mwa sheria.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *