SWAHILI โ€“ Nahodha wa Rayon Sports apinga tuhuma za rushwa baada ya kipigo kutoka APR

Sangiza iyi nkuru

Nahodha wa Rayon Sports, Muhire Kevin, amekanusha madai kwamba baadhi ya wachezaji wa timu hiyo walipokea rushwa kwenye fainali ya Kombe la Amani walipopoteza dhidi ya APR FC. Aliwaomba mashabiki na wanahabari kusitisha kusambaza uvumi huo, akisisitiza kuwa hakuna mchezaji wa Rayon aliyehusika.

Rayon Sports walifungwa mabao 2-0 na APR FC tarehe 4 Mei 2025, na kusababisha baadhi ya watu kuhisi kuwa baadhi ya wachezaji โ€“ hasa mabeki na viungo, akiwemo nahodha โ€“ hawakucheza vizuri kwa makusudi. Wengine wakadai kwamba tayari wamekubaliana kujiunga na APR FC msimu ujao.

Muhire alisema kuwa timu inapitia kipindi kigumu, lakini hiyo isiwe sababu ya kuwasingizia wachezaji mambo mabaya. Aliwataka mashabiki kuwa na subira na kuendelea kuipa timu yao moyo.

Kocha mkuu, Rwaka Claude, pia alisema hakuna ushahidi wowote wa rushwa, na akaeleza kuwa lengo lao ni kumaliza Ligi Kuu kwa mafanikio.

Rayon Sports inaongoza msimamo wa ligi kwa alama 53, na itacheza dhidi ya Rutsiro FC siku ya Alhamisi katika Uwanja wa Kigali Pelรฉ, kwenye mchezo wa 26 wa ligi.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *