Watafiti wa afya wamegundua kuwa kuna vyakula na vinywaji fulani vinavyoweza kudhoofisha mwili wakati wa tendo la ndoa, hasa kwa kusababisha unene kupita kiasi, kupunguza nguvu, na kuharibu homoni zinazohusika na hamu ya ngono.
Hii husababisha wanaume na wanawake wengi kukosa nguvu au kupoteza hamu ya kushiriki tendo.
Haya ndiyo unapaswa kuzingatia au kuepuka kwenye mlo wako wa kila siku:
1. Fanta na vinywaji vyenye sukari nyingi
Ingawa vinaweza kuleta furaha ya muda, wataalamu wanasema vinaathiri ubongo na moyo kwa kunywewa mara kwa mara. Sukari nyingi huongeza kiwango cha glucose kwenye damu, na kusababisha uchovu na kutojihisi vizuri wakati wa tendo la ndoa.
Ushauri: Badala ya kunywa Fanta mara kwa mara, chagua maji au chakula chepesi chenye nguvu asilia.
2. Viazi vya kukaanga (chips)
Chips ni tamu lakini zina mafuta mengi ambayo huathiri nguvu za kijinsia, hasa kwa kushusha ubora wa mbegu kwa wanaume. Zaidi ya hayo, vyakula vya kukaanga huongeza hatari ya magonjwa ya moyo.
Ushauri: Chagua viazi vitamu vya kuchemsha au kuoka. Vinasaidia kuzuia unene kupita kiasi na kudhibiti sukari ya mwili.
3. Kuchanganya pombe na vinywaji vya sukari
Unywaji wa pombe au vinywaji vyenye sukari nyingi—hasa vikichanganywa—huweza kupunguza hamu ya tendo la ndoa na kuathiri homoni muhimu za afya ya kijinsia.
Ushauri: Tumia kiasi, na epuka kuchanganya aina nyingi kwa wakati mmoja.
4. Pasta
Pasta ina wanga mwingi na huchukua muda mrefu kusagwa. Ukila sana, huongeza mafuta mwilini na kudhoofisha akili na mwili, hasa wakati wa tendo.
Ushauri: Kula pamoja na mchuzi wa nyanya na saladi. Usile pasta peke yake kila wakati.
5. Biskuti
Biskuti zina mafuta na sukari nyingi ambazo husababisha unene na kupunguza ustawi wa mwili wakati wa tendo, hasa kwa kuvuruga upumuaji na mzunguko wa damu.
Ushauri: Kama huwezi kuacha kabisa, kula pamoja na chakula chenye virutubisho kama siagi ya karanga au omeleti ndani ya mkate.
Vyakula vingine vinavyoweza kusababisha unene na kupunguza uwezo wa tendo ni: mayai yakiliwa kupita kiasi, nyama ya kuku yenye mafuta mengi, parachichi, na samaki wa mafuta mengi kama makayabu—ikiwa vinaliwa mara kwa mara.


