72747045_803

Moto Wateketeza Hospitali Hamburg, Watu 3 Wafariki, 50 Wajeruhiwa

Sangiza iyi nkuru

Moto mkubwa ulizuka usiku wa manane katika Hospitali ya Marien mjini Hamburg, Ujerumani, ambapo moshi ulienea hadi kwenye ghorofa zote za jengo lililoathirika.

Watu watatu wamefariki na wengine 50 wamejeruhiwa katika ajali hiyo ya moto iliyotokea katika hospitali ya kaskazini mwa Hamburg, kulingana na ripoti ya Deutsche Welle.

Moto huo ulianza baada ya saa sita usiku katika moja ya majengo ya hospitali ya Marien katika eneo la Hohenfelde. Msemaji wa idara ya zimamoto alisema kwamba moshi mzito uliingia hadi ghorofa zote za jengo hilo.

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, lakini iliripotiwa kuwa ulianzia katika kitengo cha wagonjwa wazee (geriatrics). Kikosi kikubwa cha waokoaji kilitumwa kuzima moto huo na kuwahamisha wagonjwa hadi maeneo salama.

Mapema Jumapili asubuhi, viongozi walitangaza kwamba moto huo ulikuwa umezimwa. Viongozi hao waliongeza kuwa wagonjwa waliokuwemo kwenye jengo lililoungua walihamishwa.

Baadhi ya wagonjwa waliojeruhiwa walikuwa wanatibiwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi, huku wengine wakipelekwa katika hospitali zilizo karibu.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *